NEYMAL KUHUKUMIWA KWA UKWEPAJI WA KODI
Mshambuliaji wa kimataifa
wa Brazil anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar
bado yupo kwenye headlines za ukwepaji kodi, kama ambavyo zilivyokuwa
zinawakabili mastaa wenzake wa FC Barcelona Lionel Messi na Javier
Mascherano.
Neymar ameripotiwa kukutwa
na hatia ya ukwepaji kodi wa euro milioni 56.4, kutokana na makosa
mawili ya ukwepaji wakati wa uhamisho wake kutoka Santos kujiunga na FC
Barcelona na mkataba wake Nike, makosa hayo yamefanyika kupitia kampuni
zake za (Neymar Sport e Marketing, N & N Consultoria, N & N
Administracao de Bens) kati 2012 na 2014.
Kwa mwaka 2016 pekee Neymar
anakuwa mchezaji wa pili ya FC Barcelona kukutwa na kosa hilo, aliwahi
kuhukumiwa mwaka mmoja Javier Mascherano ila adhabu yake ikabadilishwa
na kuwa faini. Sheria za Hispania zinaeleza kuwa mtu akikutwa na hatia
ya ukwepaji kodi anaweza badili kifungo na kulipa fedha.
NEYMAL KUHUKUMIWA KWA UKWEPAJI WA KODI
Reviewed by The Choice
on
1:17:00 PM
Rating:

No comments: