Gari linalojiendesha la Google lagonga basi
MOJAWAPO ya gari la Google
linalojiendesha limegonga basi moja mjini California, Marekani mwezi
uliopita. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Sio mara ya kwanza kwa gari
linalojiendesha la Kampuni ya Google kuhusika katika ajali, lakini
huenda ni mara ya kwanza kwa magari hayo kufanya ajali.
Kampuni ya Google inatarajia kukutana na
idara ya magari mjini California ili kuzungumzia kuhusu ajali hiyo na
kubaini ni nani wa kulaumiwa.
Mnamo Februari 14, mwaka huu gari hilo
ambalo lilikuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 3 kwa saa liligonga basi
moja la umma lililokuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 24 kwa saa.
Mtu aliyekuwa katika gari hilo la Google
aliripoti kwamba alidhani basi hilo lingepunguza mwendo ili kuisubiri
gari hiyo kupita hivyo basi hakuingilia kompyuta inayoendesha gari hilo.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mountain View karibu na makao makuu ya Kampuni ya Google.
Katika taarifa yake Google ilisema “Tunabeba lawama kwa sababu iwapo gari letu lisingeenda kusingekuwa na ajali
Gari linalojiendesha la Google lagonga basi
Reviewed by The Choice
on
10:09:00 PM
Rating:
No comments: