TOP 20 ya Ikulu zinazotumia magari ya kifahari duniani, Afrika zipo nchi 2 tu, Kenya ikiwemo

Kenya-Mercedes-Benz-Pullman-S600
Mtu wangu wa nguvu najua umesikia au unaelewa jinsi gari za viongozi wa juu wa serikali hususani marais zinavyokuwa na thamani kubwa kutokana na hadhi na uhitaji wa gari zenye usalama kwao. Basi mtu wangu wa nguvu katika pitapita zangu mtandaoni nikakutana na TOP 20  ya Ikulu 20 zinazotumia magari ya kifahari. Haina maana kama wengine gari zao hazina thamani ila baadhi ya hizi nchi viongozi wao wanatajwa kuamua kutumia gari hizi. Huenda ukawa hujui Afrika kuna nchi mbili tu Kenya na Morocco ndio Ikulu zake zimetajwa katika list hii. Hii ni list kwa mujibu wa therichest.com nimeisogeza kwako kama ilivyo imeandikwa na Chriss Flynn tarehe 23/01/2016
20 – Kenya0

Ikulu ya Kenya wanatajwa kutumia Mercedes-Benz Pullman S600 bei yake inatajwa kufikia dola 50,000 ambazo ni zaidi ya milioni 100 za Kitanzania
19 – Italia
Lancia-Thesis
Italia wao wanatajwa kutumia gari aina ya Lancia Thesis yenye thamani ya dola 65,709 ambazo ni zaidi ya milioni 140 za kitanzania.
18 – Japan
185
Hii ndio gari inayotumiwa na Ikulu ya Japan Toyota Century Royal thamani yake ni dola 85,500 zaidi ya Tsh milioni 180 za kitanzania
17 – Singapore
171
Serikali ya Singapore inatajwa kutumia gari aina ya Mercedes-Benz S350L yenye thamani ya dola 85,995 ambazo ni zaidi ya milioni 185 za kitanzania. 
16 – Uzbekistan
Uzbekistan-Range-Rover-Supercharged
Ikulu ya Uzbekistan wanatumia Range Rover Supercharged bei yake ni dola 103,195 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 225
15 – Morocco
Mercedes-600-Pullman
Kwa Morocco inatumiwa Mercedes 600 Pullman bei yake ni dola 120,384 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 260
14 – Korea Kusini
144
Korea Kusini Hyundai Equus VL500 (550) Limousine yenye thamani ya dola 122,180 ndio inatumika katika nchi hiyo. yake thamani yake ni zaidi ya Tsh milioni 265
13 – Norway
136
Norway wanatumia Binz Limousine yenye thamani ya dola 128,351 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 280
12 – Brunei 
Rolls-Royce-Phantom-VI
Hii inaitwa Rolls Royce Phantom VI ina thamani ya dola 148,645 ambazo ni zaidi Tsh milioni 320
11 – Ujerumani
117
Ikulu ya Ujerumani wanatumia Mercedes-Benz S600L thamani yake dola 174,890 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 380
10 – India
103
Mercedes-Benz S600 (W221) Pullman Guard thamani yake ni dola 180,000 zaidi ya Tsh milioni 390
9 – Philippines
96
Mercedes-Benz W221thamani yake dola 250,547 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 540
8 – Urusi
84
Mercedes S-Class Limousine thamani yake ni dola 251,417 zaidi ya Tsh milioni 545
7 – Malaysia
76
Maybach 62 thamani yake ni dola 394,000 zaidi ya Tsh milioni 850
6 – UK
64
Jaguar XJ Sentinel thamani yake dola 455,025 zaidi ya Tsh milioni 990
5 – Thailand 
maybach-thailand
Maybach 62 Limousine thamani yake inafikia dola 500,000 zaidi ya Tsh bilioni 1
4 – Vatican 
Mercedes-Benz-M-Class
Mercedes-Benz M-Class bei yake inafikia dola 524,990 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1.1
3 – China
35
China wanatumia Hongqi Limousine ya dola 801,624 zaidi ya Tsh bilioni 1.7
2 – USA
shutterstock_Obama-Cadillac-One
Cadillac One hii inatajwa kuuzwa dola milioni 1.5 na hutumiwa na Rais wa Marekani Barack Obama zaidi ya Tsh bilioni 3.2
1 – Malkia wa Uingereza ndio anatumia gari yenye thamani kuliko zote.
116
Bentley State Limousine inatumiwa na Malkia wa Uingereza thamani yake ni dola 15,167,500 zaidi ya Tsh bilioni 33
TOP 20 ya Ikulu zinazotumia magari ya kifahari duniani, Afrika zipo nchi 2 tu, Kenya ikiwemo TOP 20 ya Ikulu zinazotumia magari ya kifahari duniani, Afrika zipo nchi 2 tu, Kenya ikiwemo Reviewed by The Choice on 11:23:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.