ETIHAD YAPEWA TUZO YA SHIRIKA LA NDEGE LA MWAKA 2016 NA JARIDA LA AIR TRANSPORT WORLD
PRESS RELEASE
Shirika la Ndege la Etihad limetunukiwa tuzo ya Shirika la Ndege la mwaka 2016 kutoka Jarida kubwa la Air Transport World (ATW) lililopo nchini Marekani linaloandika habari za usafiri wa anga. Tuzo hii imelitambua Shirika hili kwa kuwa na timu iliyo na mikakati inayohamasisha ukuaji wa Shirika na kukuza ushikiano wake wa kipekee; katika kuleta bidhaa zenye manufaa makubwa; kujenga nguvu kazi yenye hamasa; na kujenga utetezi wa kidiplomasia wakati wa ugomvi mkali kati yao na wasafirishaji wa Wamarekani.
Shirika la Ndege la Etihad lilichaguliwa na bodi ya wahariri wa jarida hili huku kukiwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashirika zaidi ya 100 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni. Tuzo hii ilitolewa katika hafla ya chakula cha jioni iliyohudhuriwa na wadau wa sekta ya usafiri wa anga. Shughuli hii huandaliwa mara moja kila mwaka, ya mwaka huu ikiwa ya 42 tangu kuanzishwa kwake na kufanyika usiku wa kuamkia tamasha la anga la Singapore.
James Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema: “Tuzo hii ni kiashiria cha kufikia malengo tuliyojiwekea takribani miaka 13 iliyopita ya kuwa salama, kuwa shirika lenye faida na kuwa shirika lenye ubora wa hali ya juu. Inaonyesha nguvu zetu - mbinu imara za biashara, bidhaa zenye ubunifu na huduma iliyo bora zaidi inayotolewa na wafanyakazi zaidi ya 27,000 walio na ari kubwa. Nimefurahi kupokea zawadi hii kwa niaba yao, kama Shirika, tumejitahidi kutoa huduma za kipekee kwa wasafiri na tumekuza biashara yetu ili kusaidia sura ya usafiri wa anga duniani”.
Ili kustahili hii tuzo, ATW walisema Shirika lilitakiwa kuonyesha mafanikio ya kipekee katika operesheni zake, uwezo wa kifedha, huduma bora kwa wateja, usalama na mahusiano bora ya wafanyakazi. Timu ya uongozi wa juu pia ilibidi kuonyesha ubunifu na uwezo wa kuvumbua mikakati itakayoipa kampuni muonekano tofauti na nyingine.
ETIHAD YAPEWA TUZO YA SHIRIKA LA NDEGE LA MWAKA 2016 NA JARIDA LA AIR TRANSPORT WORLD
Reviewed by The Choice
on
3:31:00 PM
Rating:
No comments: