IDARA YA UHANDISI YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD MWENYEJI MKUTANO WA AE&M ABU DHABI



Idara ya Uhandisi ya Shirika la Ndege la Etihad itakuwa mwenyeji na mdhamini wa mkutano ujao wa uhandisi na ukarabati wa ndege wa mtandao wa MRO uliopo Mashariki ya Kati, Mkutano huo unaotazamiwa kufanyika mjini Abu Dhabi mwezi Aprili 26-27, 2016. Mjadala mkuu utakuwa juu ya ukuaji wa mtandao wa  MRO wenye historia isiyopungua miaka 20, wenye wadau katika sekta za – Ndege, MROs, OEMS na Wauzaji – kuwaleta pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kimasoko.

Mada mbalimbali kama maendeleo katika masoko ya usafiri wa anga huko mashariki ya  Kati, sekta ya utabiri wa masoko ya MRO pamoja na jinsi mashirika ya ndege yanajenga mahusiano na wadau wengine wa MRO.

Miongoni mwa wazungumzaji sekta inayoongoza ni Jeff Wilkinson, Makamu wa Rais shirika la ndege la Etihad kwa upande wa Ufundi alisema: " Ni furaha yetu kuwa mwenyeji wa wajumbe wa uhandisi na ukarabati wa ndege hapa mjini Abu Dhabi – kitovu kipya cha masuala ya teknolojia ya anga na usafiri kanda ya mashariki ya Kati”

Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanikisha maonyesho mengine kama haya, idara ya uhandisi ya Shirika la ndege la Etihad kwa mara nyingine tena itatoa ziara ya kituo chake kwa wajumbe baada ya kuhitimisha mkutano huo, hivyo kuwapa fursa wajumbe kukutana na timu ya uongozi ya idara ya uhandisi  pamoja na kutoa fursa ya kutembelea karakana  na warsha mbalimbali ndani ya kituo .

"Tumeandaa ziara ya kituo cha kisasa kabisa cha idara ya uhandisi ya shirika la ndege la Etihad, karakana zake  pamoja na warsha zitakazo fanyika katika kituo hicho kikubwa kuliko vyote katika mtandao wa MRO kanda ya mashariki ya kati. Hii ni pamoja na karakana sita (6) zenye uwezo wakuhifadhi hadi ndege kubwa tatu (3)  aina ya A380 kwa wakati mmoja. "

Habari zaidi juu ya mkutano huo, ikiwa ni pamoja na mjadala na wasemaji yanaweza kupatikana katika tovuti yetu ya www.airlineengineering-middleeast.com

MWISHO


Maelezo kwa Wahariri:

Uhandisi na Ukarabati ya ndege: Mahariki ya kati umeandaliwa na mtandao wa MRO



Mtandao wa MRO, sehemu ya mtandao wa anga wa Penton Wiki, ni chombo cha habari kinachoipa sauti jamii ya MRO kimataifa - watu wanaofanya kazi ya sekta ya uhandisi na ukarabati ndani ya mashirika ya ndege, MROs , OEMs, wafadhili, wauzaji na washirika wengine ndani ya sekta ya anga .



Mtandao wa MRO huleta pamoja fursa mbalimbali kujifunza habari, uchambuzi na maoni - katika magazeti, uso kwa uso pamoja na mtandaoni - katika uhandisi na ukarabati na maendeleo ya sekta ya anga.



www.mro-network.com

Twitter: @mronetwork



Kuhusu Idara ya Uhandisi ya Shirika la Ndege la Etihad
Idara ya Uhandisi ya Shirika la Ndege Etihad ni kubwa na inahusika na hudma za matengenezo ya ndege za kibiashara , kukarabati na kubadilisha (MRO) hukoa Mashariki ya Kati.
Kama kampuni tanzu ya shirika kuu la Etihad , kampuni inatoa huduma ya ukarabati mdogo hadi mkubwa masaa 24njia , mwanga na huduma kubwa za matengenezo kote saa, ikiwa ni pamoja na kubuni, kukarabati, vyumba vya ndege na sehemu nyingine za ndege, kutoka kwenye kituo chake cha hali ya juu kilicopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi Ndege.



Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad

Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.

Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na  airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
IDARA YA UHANDISI YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD MWENYEJI MKUTANO WA AE&M ABU DHABI IDARA YA UHANDISI YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD MWENYEJI MKUTANO WA AE&M ABU DHABI Reviewed by The Choice on 5:00:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.