Siku kadhaa zilizopita katika mitandao ya kijamii zilisambaa habari za kuwa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm, Gerrard Hando na Paul James (PJ) wameondoka katika redio hiyo.
Katika kipindi hicho cha Power Breakfast leo Ijumaa, Aprili 1 zimesikika sauti mpya katika kipindi hicho ambapo ni Fina Mango na Masoud Kipanya ambao wamesikika katika kipengele cha kuperuzi na kudadisi ambacho kinahusika na kupitia magazeti ya siku husika.
Baada ya kuongezeka kwa watangazaji hao, inaonyesha dhahiri kuwa Gerrard Hando na PJ watakuwa wameondoka katika kituo hicho baada ya kudumu kwa kipindi kirefu ambapo mikataba yao ilimalizika jana Machi, 31.