Picha 5:: Refa Alivyoumizwa na Mashabiki Wa Coastal Union Wakicheza na Yanga





Mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (FA Cup) kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga umeshindwa kumalizika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga kutokana vurugu za mashabiki. Mwamuzi wa pambano hilo alilazimika kulivunja pambano hilo likiwa kwenye dakika 30 za nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika huku timu hizo zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1. Hadi mchezo huo unavunjwa na mwamuzi, Yanga walikuwa wanaongoza kwa magoli 2-1. Coastal Union walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza lililofungwa na Sabo dakika ya 54 kipindi cha pili lakini Ngoma akaisawazishia Yanga kabla ya Tambwe kuiweka mbele Yanga kwa goli la dakika za nyongeza kabla ya mchezo kuvunjwa. TFF inasubiriwa kutoa muongozo juu ya mchezo huo ambao dakika zake 120 hazikumalizika
Picha 5:: Refa Alivyoumizwa na Mashabiki Wa Coastal Union Wakicheza na Yanga Picha 5:: Refa Alivyoumizwa na Mashabiki Wa Coastal Union Wakicheza na Yanga Reviewed by The Choice on 10:07:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.