Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo.

FAHAMU  KUHUSU  NDUMBA  ZA KICHAWI NA  JINSI  YA  KUJIKINGA  NAZO.

Mwandishi : Dokta. Mungwa  Kabili….0744 000 473

Nimekuwa  nikipokea  barua  pepe  kutoka  kwa  watu  mbalimbali, wakitaka  kujua  masuala  mbalimbali  kuhusu  ulozi, uchawi  na  jinsi  ya  kujikinga  dhidi  ya  uchawi  na  ulozi.

Kwa  kuwa  muda  na  nafasi  haviniruhusu  kumjibu  kila  mmoja  kwa  wakati  wake,  nitayajibu  maswali  yote  hapa  bloguni.

SWALI :   NIMESIKIA  KUWA  WACHAWI  HUWA  HAWAFI  UPESI.JE  KUNA  UKWELI  WOWOTE  KATIKA  HILO ?  NA  KAMA  NI  UKWELI, JE  NI  KITU  GANI HUWAPA  UWEZO  WA  KUISHI  MAISHA  MAREFU ?

DOKTA.  MUNGWA  KABILI  ANAJIBU :
Ni  kweli  kabisa  wachawi  wengi  huwa  hawafi  upesi  na  zipo  sababu  kuu  mbili  zinazo  wafanya  wachawi  waishi  muda  mrefu :

1.Kwanza  : NDUMBA  ZA  KINGA: Wachawi  wa  nchi  hutumia  ndumba  za  kinga, ndumba  hizo  husaidia  kuwakinga  dhidi  ya  shari  za  wanadamu   na  majini  wabaya na  hivyo kuwafanya  waishi  siko zote  walizo  pangiwa na  Mwenyezi  Mungu. Ikitokea  mchawi mwenye  kinga  hizo, amefariki  dunia, basi   anakuwa amefariki  kwa mkono  wa  Mungu mwenyewe  na  si mwanadamu. Watu  wengi  hufa  kwa mikono ya  wanadamu  waovu  na shari za  mapepo  wabaya.  Nitataja  ndumba  mbili  zenye nguvu  zinazo  tumiwa  na  wachawi.

i.  Kuna  ndumba   moja  ya  kichawi, ambayo  kwa  lugha  za  kisukuma  na  kinyamwezi  hujulikana  kama  LUFAKALE.

Ndumba hii  ya  kichawi   akichanjiwa  mtu  humkinga  dhidi  ya  shari za  wanadamu  na  mapepo  wabaya. Humfanya  aishi  kwa  kadri  Mungu  alivyop  mkadiria. Humkinga  na kumuepusha  na  shari  kama  ajali (hususani ajali za  kichawi ), kufa  kwa  kurogwa  nakadhalika.

Ndumba  hii  ina  nguvu  sana  kiasi  kwamba, mtu  aliye  chanjiwa , inapofika  siku yake  ya  kufa  roho yake  huchukua  muda  mrefu  sana  kuacha  mwili  wake. Inaweza  kumchukua mwaka  mmoja  hadi  miaka  kumi. Mtu  anakuwa anonyesha  dalili zote  za  kufa, au anakuwa  ameisha  kufa  kabisa, lakini  anakuwa  bado  anaongea.  Nikipata  nafasi  siku zijazo nitaelezea  kwa  kina  kuhusu   ndumba  hii.

ii. Ndumba  ya  pili, inatokana  na  mti  unaitwa  Msonihya . Huu ndio  mti mkuu  wa  wachawi. Mtu  huu  una  nguvu  sana  za  kichawi.  Mti  huu  hutumika kutengeneza  hirizi  ambayo  huvaliwa  mkononi  kama  bangili  au  kuwekwa nyumbani. Hakuna  pepo, jinni wala  kitu  chochote  kile  kibaya  kinaweza  kumdhuru mtu aliye  pewa  hirizi  hii.

Simba , nyoka  wa  kawaida  pamoja  na  samba  & nyoka  wa  kichawi au  mnyama  yoyote  yule  hawezi  kumdhuru.

2. NDUMBA  ZA  KUWAWEZESHA  KUONA  MAMBO  YATAKAYO  TOKEA   MBELENI.

Wachawi wa  nchi  wanazo  ndumba  zenye  uwezo  wa  kuwasaidia  kujua  mambo  yatakayo  tokea   mbeleni, hivyo basi  kama  kuna  hatari  yoyote  ile  inaenda  kutokea  kesho yake kama  vile  ajali  au  shari  yoyote  ile nakadhalika, wao  wanakuwa  wameshajua  siku  moja  kabla  na  hivyo  wanakuwa  na  nafasi ya  kuchukua  tahadhari mapema.

JINSI  WANAVYO  FANYA  ILI  KUWA  NA  UWEZO  WA  KUONA  MAMBO  YATAKAYO  TOKEA.

Zipo  njia  mbalimbali  wanazo  tumia, ili  kupata  uwezo  wa  kuona  mambo  yatakayo  tokea  mbeleni, lakini  kati  ya  njia  hizo  njia  ifuatayo  ni  maarufu sana  miongoni mwa  wachawi na  walozi.

i. Wanachukua  ubongo  wa  fisi

ii.  Wanachukua  ubongo  wa  kunguru

iii. Wanachukua  ubongo  wa  ndege  anaitwa  Mbesi. Ndege huyu  hupatikana  mtoni  na  chakula  chake  kikuu  ni  mizoga ya  ndege, wadudu, samaki na  wanyama. Katika ulimwengu  wa wachawi, ndege  huyu  hujulikana  kama  mtaalamu  wa  kugundua  mahali  ilipo mizogo  iliyo  kufa.

Kwa  mfano   tuchukulie  mkoa wote  wa  Dar  Es  Salaam  ni  pori,  huyu  ndege  yupo  mbagala halafu  maeneo  ya  msasani  kuna  ndege,samaki,wadudu  au mnyama  amekufa, basi  usiku wa  siku  hiyo  ndege  huyu  ataota  mahali  ulipo mzoga  huo, na  kesho  yake  atapaa  moja  kwa  moja hadi  sehemu  ulipo mzoga  huo  na  kuufanya  kuwa  kitoweo  chake.

Vitu  vyote  hivyo  hapo  juu  hukaushwa  na  kusagwa  kwa  pamoja  na  kisha  kuchanganywa  na  ndumba  tatu  za  kichawi  ambazo  sitazitaja hapa kwa  sababu  maalumu.

Baada  ya  hapo,  mchawi  husika  atachanjiwa  ndumba  hizo  kichwani pamoja  na  kwenye  zote  nne  za  mwili.

Basi, mchawi  huyo  anakuwa  na  uwezo  wa  kuona  ndotoni  kila  kitu  kitakacho  tokea kesho  yake  na  kuendelea.

SWALI NAMBA  MBILI :  NASIKIA  WATU  WANAZUNGUMZA  KUHUSU  DUDUMIZI. JE  DUDUMIZI  NI  NINI  NA ANATUMIKAJE  KATIKA  UCHAWI

DR. MUNGWA  KABILI  ANAJIBU ;
Dudumizi  ni ndege  anaye  patikana  porini. Katika  ukanda  wa  Pwani, ndege  hawa  wanapatikana  kwa wingi  sana  katika  mapori ya  Bagamoyo   mkoa wa  Pwani,  Kisarawe  vijijini  ( Hususani  katika vijiji  vya  Mwaneromango, Nzenga  na  Msanga ) pamoja  na  wilaya  ya  Pangani  mkoani  Tanga.

Ndege hawa  wana  macho mekundu, mkia  mrefu pamoja  na  kucha  ndefu  sana.

Dudumizi  hula wadudu, mijusi, nyoka, mayai,makinda, matunda, mizoga  na wanyama  wadogo pia.

Dudumizi  wengi  wana  mabawa yenye  rangi  ya  kahawia  nyekundu  na  kichwa  cheusi.  Lakini  pia  wapo Dudumizi  wenye  mkia  wa  rangi  ya  shaba, Dudumizi  weusi,Dudumizi wenye  koo  lenye  rangi nyeusi, Dudumizi  wenye  kichwa  chenye  rangi  ya  buluu, pamoja  na  Dudumizi wenye  nyushi nyeupe.

MAAJABU  YA  DUDUMIZI.
Dudumizi  ni ndege  mwenye maajabu mengi  sana, kwa  muwa  muda  hauturuhusu, leo nitataja  mawili  tu.

AJABU  LA  KWANZA :  Ana  uwezo  wa  kujifungua  kamba  mwenyewe. Kwa  mfano, ukienda  kwenye  kiota  cha  Dudumizi, halafu  ukawafunga  makinda  wa  Dudumizi kamba  kisha ukafunga  na  kwenye  mti. Kesho  yake  asubuhi  unakuta ile  kamba  imejifungua  yenyewe . Ukimnchukua  Dudumizi ukampeleka  nyumbani  kwako, ukamuweka  kwenye  banda, halafu ukamfunga  kamba  akiwa  bandani, ukafunga  banda halafu kamba  hiyo  ukaenda  kuifunga  kwenye  mti  au  kitu  chochote  kile, kesho  yake  unakuta Dudumizi  amefungua  hiyo kamba na  kuondoka, hata  kama  kamba  hiyo  itakuwa  kubwa  na  nzito  kwa  kiasi  gani.


AJABU  LA  PILI : Kwa  kawaida  Dudumizi  hutaga  mayai  kati  ya  mawili  hadi  matano. Dume  la  Dudumizi  ambalo  huwa  dogo  kwa  umbo  kuliko  jike, ndio  linalo  hatamia  mayai na  kutunza  makinda.

JINSI  WACHAWI  WANAVYO  MTUMIA  NDEGE  DUDUMIZI.

Katika  ulimwengu wa  wachawi, Dudumizi  ana  matumizi  mengi sana kichawi. Leo  nitataja  mawili tu  kwa  sababu  ya  muda.

1.Kamba  iliyo  tumika  kuwafunga  Dudumizi na  ikajifungua  yenyewe, ikichanganya  na  ndumba  za  kichawi  pmaoja na  vizimba  vyake, hutumika  kuwafungua  kichawi, watu  walio katika  vifungo  mbalimbali  vya kichawi  kama  vile  vifungo  katika biashara, vifungo  katika  mapenzi na  ndoa, vifungo  katika  rizki , vifungo  vya  mizimu,  nakadhalika.

2. Dudumizi  hutumika, kutengeneza  ndumba maalumu kwa  wale  wanawake  wanao penda  kuwa inamisha  waume  zao.

SWALI  NAMBA  TATU: JE  NI KWELI  KUWA  WACHAWI  WANA UWEZO WA KUMTIA  MTU  MIKOSI NA  KUFUNGA  RIZIKI  YAKE?

DOKTA.MUNGWA  KABILI  ANAJIBU ;
Ni kweli  kabisa,wachawi  wana  uwezo  wa  kumtia  mtu  mikosi . Zipo  njia  mbalimbali  wanazo  tumia  wachawi  katika  kuwatia  watu  mikosi, ila kutokana  na  ufinyu  wa  nafasi, nitaelezea  moja  hapa ;

Katika  njia  hii, wachawi  wakitaka  kumtia  mtu  mikosi, hufanya  mambo  yafuatayo :

i. Wanachukua  hela  ambayo  haitumiki

ii.  Mavi  ya  mbwa  mweusi ambayo  ameyanya  usiku

iii.Mkaa  ulio kwisha  tumika, ambao  umetumika  mahali  ambapo  watu  hawalali  kama vile  kilioni  au  kwenye  bara  na migawaha  inayo  kesha lakini  mara  nyingi, huchukua  mkaa  wa  kilioni.

iv. Mavi  ya  ndege  anaitwa  Mumbi. Huyu ndege  aitwae  Mumbi  anapatikana  porini. Anafanana  sana  na  bata  na  ana  puyanga  la rangi  nyekundu.

v.Shahidi la  kaburini  pamoja  na  ndumba  zingine  za  kichawi

vi.Kitu  chochote  cha  mtu  aliye  kusudiwa  kutiwa mikosi  kama  vile  picha  yake, mchanga  alipokanyagia, mate, kucha, au chochote  kile.

Baada  ya  hapo, mchawi  huyo  atakwenda  kaburini  usiku  wa  manane  na  kuvizika  vitu  vyote  nilivyo  vieleza  hapo  juu, huku  akisema  maneno  ya  kichawi ambayo  siwezi  kuyataja hapa. Basi  mtu  aliye  kusudiwa  na  uchawi  huu, kama  hana  kinga, ata andamwa  na  mikosi mikubwa  na  mizito  katika  maisha  yake  yote.

SWALI NAMBA  NNE  :  DOKTA, NINAPENDA  KUJUA  NINI  KINGA  DHIDI  YA  UCHAWI? NIFANYE  NINI  ILI  UCHAWI  USINIDHURU ?

DOKTA  MUNGWA  KABILI  ANAJIBU:
Kama  wewe  ni  Muislamu, uwe  mtu wa  swala  sana, kufanya  duwa na  visomo ( Ruqiya)  na  kutoa  Dhaka na swadaka  kwa  mola  wako, na  kama  wewe  ni  Mkristo, basi  uwe mtu  wa kusali  sana, kufunga  na  kuomba  bila  kusahau  kutoa  sadaka  na  fungu  la  kumi  kwa  Mungu  wako.

Lakini  kama  unajijua, hauwezi  kufanya  mambo  niliyo  yataja  hapo  juu, basi  unatakiwa  kupata  kinga  ya  mwili  wako.

Zipo  kinga  nyingi zenye  nguvu dhidi  ya  uchawi  na  ulozi. Zipo  Kinga, mchawi  akikutupia  uchawi  unamrudia  mwenyewe ana  kufa  papo hapo  au  anapooza  kwanza kwa muda mrefu  kisha  anakufa pia zipo kinga ambazo  mchawi ,  akitaka  kukutupia  uchawi, anashindwa  kukuona  katika rada zake  za  kichawi.

Hii  ni  kinga  muhimu  sana na haiishii  kukukinga  mwili wako  pekee.Inakinga nyumba, biashara, kiti  cha  ofisi  nakadhalika.

KINGA  HII  HUJULIKANA, KAMA  KINGA  YA  KUFICHA  KIVULI  CHAKO.

Inaitwa  Kinga  ya  Kuficha  kivuli, kwa  sababu  wachawi  wanapo taka  kumloga  mtu, huchukua  na  hushambulia  kivuli  chake. ( HAPA  SIZUNGUMZII  KIVULI  CHA  JUANI, NAZUNGUMZIA  KIVULI  CHAKO  CHA  KIROHO, YAANI  NAFSI YAKO )

Bila  kuona  kivuli  chako, wachawi  hawawezi  kukuloga.

Kinga  hii  hukupa  uwezo  wa  kutokuonekana  kwenye  rada  za  wachawi. Kwao  unakuwa  ni  sawa  na  mtu  aliye  kufa tu, kwa sababu  mtu  aliye  kufa kivuli  chake  hakionekani  na  pia hawezi  kurogwa  na  uchawi  wa  aina  yoyote  ile.

JINSI  YA  KUFICHA  KIVULI  CHAKO  KISIONEKANE  NA  WACHAWI.

i.  Chukua  nywele  za  saluni
ii. Chukua  mzizi  wa  mti  ulio  katisha  njia
iii. Chukua  tawi  la  mti  unaitwa  Ututukanga. Huu  mti  wa  Ututukanga  unapatikana  porini na  huwa  linaonekana  shina  lake  na  matawi  yake  tu, lakini  mzizi  wake huwa  hauonekani.

iv. Unachukua  mti   unaitwa  Msonihya

v.  Unasaga  pamoja  na  mti  unaitwa  mwavi.

vi. Baada  ya  hapo  unachukua  kuku  mweusi, unamfunga  kwenye kitambaa  cheusi  bila  kumchinja, unachukua  chungu  cheusi, unamuunguza  mpaka  anakuwa  mkaa, halafu  unamsaga  pamoja  na  miti  iliyo  tajwa  hapo  juu, unachanganya  na  mafuta  ya  simba.

vii. Unachukua  buja ama  dulya  la  ugali  wa  kilioni

viii. Kamba  ya  kitanda  alicho  lalia  maiti, au kama  maiti  ipo  kwenye  nyumba  ya  nyasi, unachomoa  nyasi  wakati  maiti  imo  ndani.

ix.  Unachimba  mzizi  wa  mti  unaitwa  mputika  bila  kivuli chako  kugusa mti..

x. Unaunguza  vyote  kwa  pamoja  ukiwa  na  kaniki  nyeusi  bila  kuvaa  nguo  yoyote  usiku wa  manane

xi. Unaipika  njia  panda pamoja na  mafuta  ya  mti  mmoja  wa  porini  ambao  jina  lake  linahifadhiwa  hapa.

Baada  ya  hapo, mtu  atachanjiwa  na  kuongeshwa pamoja  na  kufanyiwa  tambiko  maalumu.

Basi wachawi  watakuwa  wakijaribu  kutaka  kukutupia  uchawi, wanakuwa  hawakauoni  kwenye  rada  zao za  kichawi

SWALI NAMBA  TANO :  HABARI  YAKO DOKTA. NASUMBULIWA  SANA  NA  WIZI NYUMBANI  KWANGU. JE  IPO  NDUMBA YA  KUMKAMATA  MWIZI ?

DOKTA  MUNGWA  KABILI  ANAJIBU :
Zipo  ndumba  nyingi  za  kuwakamata  wizi. Leo  nitataja  ndumba  rahisi  kabisa  ya  kumkata  mwizi. Ukifanya  ndumba  hii, basi  mwizi  atajileta  mwenyewe  na  kuomba  msamaha.

i. Unachukua  kinyonga akiwa mzima

ii. Unaponda  majani ya  kisamvu

iii.Unachukua  na  changarawe  za  njiani  ambazo, hutembea  mvua  ikinyesha.

iv.                Huyo  kinyonga  unamuweka  kwenye  hayo majani  ya  kisamvu pamoja  na  hizo  changarawe, unafunga  kwenye  kitambaa  cheusi  halafu  unafunga  jikoni, kwenye sehemu  inayo  toka  moshi. Utamuacha  hapo  kwa muda  wa  siku  saba.

Baada  ya  siku  sita, unamtoa  hapo kwenye  moshi, unasaga  ukiwa  umefumba  macho  halafu  unaenda  kuvifunga  kwenye  mti  kwa  muda  wa  siku  saba. Kabla  siku  saba hazijaisha, mwizi  wako  atarudi  mwenyewe. Na  kama  mwizi  yumo  humo  humo  ndani, atajisalimisha  mwenyewe  mara  moja.

Hii  dawa  moja  tu, lakini  zipo  nyingine  nyingi.

SWALI NAMBA  SITA : DOKTA   NASIKIA  WACHAWI  WANA  UWEZO  WA  KUTUMIA  UCHAWI  KUMSHIKA  MWANAUME  KIMAPENZI . JE  NI  KWELI? NA  WANAFANYAJE  FANYAJE ?

DOKTA. MUNGWA  KABILI  ANAJIBU.
Katika masuala  ambayo  uchawi una  ishi na  kutawala  basi  ni  suala  la  mapenzi.

Asilimia  kubwa  ya  watu  wanao  enda  kwa  waganga, huenda  huko  kwa  sababu  ya  mapenzi  au  kwa  sababu  ya  mambo  yanayo  sababishwa  na  mapenzi.

Uchawi  wa  mapenzi  upo  wa  aina  nyingi  sana. Nikisema  nianze  kutaja na  kuelezea  kwa  kila  aina  ya  uchawi  na  ulozi  katika  mapenzi  hapa, sitamaliza  kwa  sababu  upo uchawi  wa  aina  nyingi  sana.

Nitataja na  kuelezea kwa  ufupi  sana, aina  chache  za  uchawi  katika  mapenzi, halafu  nitaelezea  aina  moja  ya  uchawi  wa  mapenzi  ambao  ni uchawi  hatari  na  wenye nguvu  sana.

KUMSHIKA  MWANAUME  KATIKA MAPENZI ;  Kumshika  mwanaume  katika mapenzi, wachawi  huchukua  njiwa  wawili  jike dume  walio zaliwa  kiota  kimoja pamoja  na  kiota  chawe, kisha  njiwa  hao huchinjwa , hupasuluwa  na  mioyo  yao  hunyofolewa, huchemshwa  kwenye  mafuta  ya  mti  mmoja  unapatikana  porini, halafu husagwa  hadi  kuwa  unga  unga. Baada  ya  hapo huchukua  njugu  mawe  nyeusi  moja, huchanganya  na  mti  unaitwa  mlama, pamoja  na  miti  mingine  mitatu  ya  porini, kisha   husagwa  pamoja  na ile  mizoga  ya  njiwa.

Vyote  hivi  kwa  pamoja, huchanganywa  na  vizimba  vitatu  vya  ndumba  za  kichawi, halafu  mwanaume  huwekewa  kwenye  chakula, basi mwanaume huyo atakuwa  hasemi chochote  kwa  mwanamke  huyo.Mwanamke atakuwa  mama  ake  atakuwa  baba  ake. Ni uchawi  mbaya  sana huu.

KUMFANYA  MWANAUME  ASIENDE  NJE  YA  NDOA :
Kumfanya  mwanaume  asiende  nje  ya  ndoa, wachawi  huchukua kamba  ya  mbuzi, moyo  wa  kondoo, mti unaitwa  INAMA  NIKUCHUME (  Mti  huu  unapatikana  Kigoma tu, na  watu  wa  kigoma  ndio  huuita  jina  hilo), mti  unaitwa Inyazya  kisha  vinasagwa  kwa  pamoja  halafu  vinachanganywa  na  nta ya  nyuki, kisha  wanatafuta  kucha, au nywele, au ndevu, au uzi wa nguo yake yoyote, halafu vinakaangwa  kwa  chumvi  ya  mawe  pamoja  na  vizimba  vya  zote  \nilizo zitaja  hapo juu, kisha vinafungwa  kwenye kitambaa chekundu, halafu  vinafukiwa  mlangoni  au  kwenye  mti  wowote. Basi mwanaume  huyu hawezi kwenda  nje  ya  ndoa  yake.

MWANAUME AKUONE  WEWE TU KILA ANAPOKUWA  NA  MWANAMKE MWINGINE : Wachawi  hutchukua   maji ambayo  mwanamke  ametumia  kunawa  uso wake kisha huchanganya  na  ndumba  13  za  kichawi  pamoja  na  vizimba  vyake kisha  kutengeneza  ndumba  itakayo  mfanya  mume  wa  mwanamke  huyo kuwa  anaumuona mke  wake  wakati  wote na pia  kuwa   anaona kama  anatokewa  na  mke  wake  kila  anapo  kuwa na  michepuko.

KUMFANYA  MUME  AKUPE  MSHAHARA  WAKE  WOTE  AU PESA  ZAKE ZOTE  KILA  AKIZIPATA: Uchawi  huu  umewalostisha  wanaume  wengi  sana. Hapa mchawi  anacho chukua  manii  za  mwanaume aliye  mkusudia, ana changanya  pamoja  na  baadhi  ya  vitu  alivyo pewa  na  mwanaume  huyo, halafu  vinaenda  kutengenezwa kichawi kwa  kutumia  ndumba  za  kichawi, basi mwanaume  huyo  atakuwa  kila  akipata  mshahara wake  anapeleka  zote  kwa  mwanamke  huyo. Asipojistukia  mapema, anaweza  uza  kila  kilicho  chake.

KUMVUTA  MPENZI :  Ipo miti  mitatu  inapatikana  porini, miti  hutumika  kumuita  kichawi  mwanamke  au  mwanaume  aliye  kusudiwa.

KUMTEGA  DAWA ZA  MAPENZI  MWANAMKE  AU  MWANAUME.
Chaurembo  kaenda  kwa  wachawi, na  kuwaomba  wampe  msaada  wa  kichawi  ili  aweze kumteka  kimapenzi Ndugu., Maridadi.

Wachawi  watamchukua  Chaurembo, watampa  ndumba  za  aina  tatu. Ndumba  ya  kwanza, atachanjiwa, kichwani  na katika  pembe  zote  za  mwili wake. Ndumba  ya  pili  atatumia kunywa, na  ndumba  ya  tatu  atatumia  kuoga  na  kuchoma.

Sikui  tatu  baada  ya kuanza  kutumia  ndumba  hizo, Chaurembo  atamuota  Maridadi anapita  katika  sehemu  ambayo  Chaurembo  anaifahamu.  Chaurembo atatakiwa  kuikariri  ndumba hiyo.

Kesho  yake, saa  saba  mchana, Chaurembo atatkiwa  kwenda  hadi  mahali  alipo  muona  Maridadi akiwa  anapita,akifika  katika  eneo  hilo, atatakiwa  kumwaga  dawa  aliyo pewa.

Maridadi  lazima  atapita  katika  eneo hilo, na  akipita  tu, basi  anakuwa  amenasa  kwenye  penzi la  Chaurembo.

Maridadi  atamtafuta  Chaurembo  kwa  udi  na  uvumba na  atafanya  kila  kitu  anacho kitaka  Chaurembo.

Huu  ni  uchawi  mbaya sana  na  hutumika  hata  katika  mambo  yasiyo  ya  mapenzi.

SIKU NYINGINE  NITAELEZEA  KWA  UREFU  SANA  KUHUSU  UCHAWI  MBALIMBALI  UNAO  TUMIKA  KATIKA  MAPENZI.

SWALI NAMBA  SABA : JE NI KWELI  WACHAWI WANA  UWEZO  WA  KUWAACHANISHA  WAPENZI  KWA  KUTUMIA  UCHAWI.
 
DOKTA  MUNGWA  KABILI  ANAJIBU :
Ni kweli kabisa, wachawi  wana  uwezo wa  kuwaachanisha  wapenzi. Mke na  mume  walio  ona  kwa  sherehe  ya  mamilioni  wanaweza  kuachana  ndani  ya  wiki  moja.

Zipo njia  nyingi sana  wanazo  tumia, ila  leo  nitaitaja  moja:

i.Wanachukua  mti  unaitwa  mpuga mbu.

ii. Mkia  wa  ndege  wa  porini  anaitwa  katyente

iii. Picha  ya  mke na mume  walio  kusudiwa pamoja  na  majina  yao.

iv. Wanachanganya  na  vizimba  vyake.

v. Vitu vyote  hivyo  vinasagwa  kwa  pamoja, kisha  vinakaangwa  kwa  kutumia  chumvi  ya  mawe, halafu vinaen da  kuchomwa  jalalani.

Hata  kama  wanapendana  vipi,wote  wataachana.

Ndumba  hii  ndio  inayo  tumika  pia  kushusha  thamani  ya  cheti  cha  mtu. Hata  kama  amesoma  vipi, hawezi  kupata  kazi  kama  akifanyiwa  uchawi  huu.

Kwa  leo  naomba  niishie  hapo, kesho  nitaendelea  tena  na  makala  haya.

MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  DOKTA. MUNGWA KABILI, MTALAAMU  ALIYE  BOBEA  KATIKA  MASUALA  YA  ULIMWENGU USIO ONEKANA. ANAPATIKANA  JIJINI  DAR  ES  SALAAM, KWA  SIMU NAMBA 0744 000 473.
Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo. Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo. Reviewed by The Choice on 9:34:00 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.